Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza mbele ya Tume ya Rais ya kukusanya maoni ya Maboresho ya Taasisi za Haki Jinai Tanzania , Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Mohammed Chande Othman ( kulia kwa makamu) na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Ombeni Sefue. Tume hiyo ilifika ofisini kwa makamu Migombani mjini Zanzibar kupokea maoni
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kuna haja ya Tanzania kuitumia
fursa ya kuundwa Tume ya Rais ya Kuborosha Taasisi za Haki Jinai, nchini
kupendekeza kuandaliwa mfumo bora utakaounda chombo rasmi na kuandaa sera bora
itakayosimamia vyema kimamlaka masuala
yote ya Haki jinai Tanzania.
Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini
kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na Wajumbe Tume hiyo iliyofika ofisini kwa Makamu kupokea maoni ya Mhe. Makamu kuhusiana na
maboresho yanayohitajika katika taasisi za haki jinai na mfumo wa mahakama
Tanzania.
Amefahamisha kwamba Tanzania kwa
sasa inaonekana hakuna mfumo na sera rasmi za kusimamia taasisi za aina hiyo na
kwamba ni jambo jema Tume hiyo kupendekeza kuundwa mfumo rasmi na chombo kimoja chenye mamlaka kubwa
pamoja na kuandaliwa sera itakayosimamia masuala hayo kwa wepesi na kusaidia
upatikanaji wa haki kwa jamii.
Mhe. Othman amesema kwamba hivi sasa
utaratibu uliopo Tanzania ni mapungufu makubwa ambayo haina uwezo na haioneshi
kuwepo utaratibu bora utakaosaidia watanzania kuendesha kwa wepesi taaisi na mfumo
huo sambamba na kuzuia kujirejea rejea kwa makosa ya jinai ya aina mbali mbali
yanayotendeka nchi.
Mhe. Makamu amesema maboresho mbali
mbali yaliyofanyika katika mfumo wa sekta ya seheria nchi bado hayajakidhi haja
na matarajio ya nchi kuwa na chombo kimoja kinachosimamia masuala yote muhimu ya haki
jinai kwani yaliyofanyika yalizingatia
zaidi urekebishaji wa kitaasisi kuliko mfumo unaohitajika sasa.
Mhe. Othman ameongeza kuwa Tanzania itakuwa imefanya jambo kubwa sana iwapo itatambua kwamba inahitajki kujenga upya mfumo na utaratibu wake wa haki jinai ili kuondoa tatitizo la sasa lililopo.
Amefahamisha kwamba mfumo wa sasa
pia unaruhusu makosa makubwa kutendwa na watu wenye nyadhifa, kubwa huku
utaratibu na uwezo wa upelelezi wa polisi ukiwa dhaifu kutokana na kujengwa
kisiasa kuliko kiuweledi zaidi, jambo ambalo athari inarudi katika kuzuia na
kupeleleza makosa mbali mbali ya jinai na hivyo kulazimika kutumia maelekezo
ya viongozi wa siasa.
Mhe. Othman amesema mfumo huo wa
polisi kupokea maelekezo ya kisasa inalifanya jeshi hilo kukosa na kujenga
weledi katika upelelezi wa makosa huku
kazi hiyo ikiwa ni ya kitaalamu zaidi kuliko ya siasa.
Amesefahamisha kwamba kutokana na
hali hiyo kunahaja ya kutathimini Idara za Upelelezi katika jeshi la Polisi
kwamba iendelee kubakia ndani ya jeshi hilo ama iwe mamlaka mbali na jeshi la
polisi linaloweza kufanya kazi zaidi ya kupeleleza kwa weledi mkubwa makosa
tofauti ya jinai.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba
kwamba hasa katika vipindi vya uchaguzi
mfumo ulipo sasa wa polisi huendelea kupokea amri za wanasiasa na hivyo
kuwafanya polisi kuendelea kutumika vibaya kinyume na malengo na matarajio ya
jamii ya watanzania jambo ambalo ni
tatizo kuwepo hali hiyo.
Kuhusu Taasisi na
Mamlaka kama za kuzuia rushwa , Tume ya Kuzuai na Kupambana na madawa ya
kulevya na mamlaka nyengine za namna hiyo mhe. Othman amesema
kwamba kwa mazingira ya Tanzania ni vyema
kuundwa kwa kuungwa pamoja chini ya chombo maalum kitakachokuwa na uwezo
wa kitaalamu na rasilimali za kutosha za
kushuhulikia mambo maalum ya
namna hiyo chini ya maadili na kuweka wepesai zaidi kiutendaji.
Eneo jengine ambalo mhe. Othman
alilizungumzia ni kuhusu masuala ya kitaalamu kama vile kwa Mkemia Mkuu, madaktari
hali ilivyo sasa hawakutengenezwa kwenda kusaidia katika upatikanaji wa haki
mahakamani lakini hutazama eneo la utaalamu zaidi katika viwango vyake vya
Kitaasisi visivyomunganiko huku kukiwa hakuna mamlaka ya juu zaidi ya kusimamia
zaidi.
Mapema mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mohammed Chande Othman amesema kwamba tume hiyo inaendelea na kutekeleza jukumu lake la kukusanya maoni na taarifa kupitia wadau mbali mbali wakiwemo viongozi taasisi za haki jinai na wengineo kwa njia ya mikutano , madodoso pamoja na maandishi ili kuwezesha kukusanya maoni na kuishauri serikali namna bora ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment