Habari za Punde

Serikali Yaipongeza Kampuni ya TIGOZANTEL Kwa Kufikisha Huduma Bora za Mawasiliano kwa Jamii

 

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dr Khalid Salum Mohamed ameipongeza Kampuni ya Mawasiliano ya TigoZantel kwa namna inavyojipambanua katika kuimarisha huduma za mawasiliano kwa Wananchi

Waziri Dkt Khalid ameeleza hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Iftari ya pamoja iliyoandaliwa na Kampuni ya TigoZantel na kufanyika katika Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar

Dkt Khalid amesema kampuni hiyo imekua karibu zaidi na jamii katika kuimarisha huduma za mawasiliano kwa kushrikiana na serikali pamoja na mfuko wa mawasiliano kwa wote,  jumla ya minara 45 yamejengwa Unguja na Pemba hasa katika maeneo ambayo awali huduma za mawasiliano zilikua ndogo

Ameongezea kuwa kampuni ya Zantel imekua mstari wa mbele katika kuongeza pato la Taifa pamoja na kurahisha huduma mbalimbali za ufanyaji wa miamala hasa kwa wakulima wa zao la Karafuu ambalo ndio za kubwa la Kiuchumi Visiwani Zanzibar

Aidha ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuanza kuboresha huduma za mawasiliano ya Internet yenye kasi ya 5G ambayo imeshaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya visiwa hivyo

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi, Afisa Mkuu wa Fedha Kampuni ya TigoZantele CPA Innocent Rwetabura amesema kwa kuthamini mchango mkubwa wa wateja wa TigoZantel kampuni hiyo imeamua kujumuika kwa pamoja katika ftari hiyo ambayo itakua sehemu ya kuendeleza umoja na mshikamano kati ya Kampuni yao na Wateja wake

Kupitia jukwaa hilo amewahakikishiwa wateja wote kuwa kampuni hiyo itaendelea kuweka mazingira bora ya utoaji wa huduma za mawasiliano ikiwemo matumizi ya haraka ya Internet yenye kasi ya 5G

Ftari hiyo imewajumuisha viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Viongozi wa Ofisi ya Mufi wakiongoza na Mufti Mkuu Shekh Saleh Omar Kabi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na wanachi mbalimbali

Afisa Mkuu wa Fedha Kampuni ya TigoZantele CPA Innocent Rwetabura amesema kwa kuthamini mchango mkubwa wa wateja wa TigoZantel kampuni hiyo imeamua kujumuika kwa pamoja katika ftari hiyo ambayo itakua sehemu ya kuendeleza umoja na mshikamano kati ya Kampuni yao na Wateja wake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.