Habari za Punde

Uwekezaji wa Bandari ya Tanga Kuwezesha Kukusanya Bilioni 5 - Naibu Waziri Mwakibete

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete akizungumza wakati wa ziara yake katika Bandari ya Tanga kulia ni  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi

Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete 



Na Oscar Assenga, TANGA.

MATUNDA ya uwekezaji katika Bandari ya Tanga yameanza kuonekana baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete kueleza kwamba Bandari nhiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya Sh.Bilioni 5 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.


Mwakibete aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja kutembelea Bandari hiyo ambapo alisema kwamba mapato hayo yametokana na kukamilika kwa Gati hatua ambayo imesaidia kuongezeka Kwa shehena ya meli za mizigo.

Alisema kwamba hayo ndio mafanikio yaliyotokana na uwekezaji wa Takribani na Sh.Bilioni 429 uliofanywa na Serikali katika Bandari ya Tanga ambao umewezesha kuongezeka kwa shehena ya mizigo hatua ambayo imepeleka kuongezeka kiasi cha mapato hayo.


“Hii ni kazi nzuri ya uwekezaji ambao umefanywa na Serikali hatua ambayo imeleta manufaa makubwa katika Bandari ya Tanga hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kutokana na kuwa na uweke"Alisema


Katika hatua nyengine,Naibu Waziri huyo alitoa muda wa mwezi mmoja kwa shirika la Reli Tanzani (TRC) kuhakikisha wanajenga miundombinu ya reli katika bandari ya Tanga ili kurahisha huduma za usafirishaji wa mizigo inayoshushwa kwenye bandari hiyo kuelekea maeneo mbali mbali ya nchi.


Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi alisema ndani ya kipindi Cha miezi mitatu wamepokea Meli kubwa tano ambazo zimebeba zaidi ya shehena ya mizigo Tani 130,000 .


Hata hivyo alisema kutokana na uingiaji wa Meli kubwa umesaidia kuwezesha ajira za muda mfupi 100 zimeweza kupatikana .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.