Habari za Punde

Dkt.Chana Afungua Maonesho ya Sanaa kwa Nchi za Ghuba

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana  Mei 26, 2023 Jijini Dar es Salaam, amefungua maonesho ya Sanaa za Ufundi yanayojumuisha nchi za Ghuba (Gulf Countries) pamoja na wenyeji Tanzania ambayo yatafanyika kwa siku saba.

Mhe. Chana amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya kufanya shughuli za  Utamaduni na Sanaa ambapo katika Mtaala wa Elimu unaoboreshwa, sekta hizo zitakuwa miongoni mwa masomo yatakayoingizwa kwenye mtaala.

"Katika utafiti uliofanywa  mwaka 2012/13, Sekta hii ya ubunifu imeajiri  Watanzania wapatao milioni 6 na kuchangia katika Pato la Taifa, ambapo mwaka 2021 ilichangia kwa asilimia 19.4", amesema Mhe. Chana.

Awali Mwenyekiti wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Bw. Adrian Nyangamale amesema maonesho hayo yanajumuisha wachoraji kutoka nchi mbalimbali za Ukanda huo, Tanzania ikiwa mwenyeji ambapo amewataka Watanzania kujitokeza kuona ubunifu ulioneshwa na Wasanii hao na kuwanga mkono.

Maonesho hayo yanajumuisha nchi za Oman, Saud Arabia, Kuwait, Bahrain Yemen, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu na wenyeji Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.