Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma Mei 26, 2023 katika Ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam ameshiriki Tamasha la Muziki la Bongo Flavor Honors lenye lengo la kutoa heshima kwa wakongwe wa muziki huo.
Mhe. Mwinjuma ameungana na wasanii wa muziki huo akiwemo Msanii JayMoe kutoa burudani kwa mashabiki waliokuepo.
Wasanii wengine walitoa burudani ni Msanii Sugu, Mchizi Mox, Dully Sykes na wengine.
No comments:
Post a Comment