Habari za Punde

Kuwajengea Uwezo Vijana Walioko Vyuoni na Wanaomaliza Vyuo Kuwaunganisha Shughuli za Kibiashara

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema ni jambo jema kuona vijana wanazitumia fursa za kitaaluma ili waweze kufikia malengo yao.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kuwajengea uwezo vijana walioko vyuoni na wanaomaliza vyuo na kuwaunganisha na shuhuli za kibiashara katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Abla Beit Ras Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo wanahakikisha wanatumia kila namna ili kuhakikisha vijana wanapata fursa mbalimbali za maendeleo.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmin Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Association of students in economics and Business AISEIC ndugu Richard Evarist amesema, taasisi yao ina lengo la kukuza na kuamsha Ari kwa vijana ili kuweza kuwa viongozi bora kwa vitendo.
Amesema lengo la mkutano huo ni kuwatengeneza vijana waweze kijiunga na vyuo na kuweza kujitegemea wenyewe kwa kipindi chote Cha masomo pia kuhakikisha wahitimu hao wanakuja kuwa viongozi wazuri wa badae.
Akizunguzia suala la Elimu hasa ya juu amesema, ni kuhakikisha wanatengeza vijana kuweza kujitegemea wenyewe mara wanapohitimu Elimu za juu.
Akisema machache Mkurugenzi wa rasilimali watu kutoka benki ya CRDB bwana Godfrey Kasigwa amesema benki hiyo ipo mstari wa mbele kuhakikisha wanawaunga mkono Wanafunzi mbalimbali hasa wa Elimu ya juu ili taifa lizalishe wataalam mbalimbali wazalendo.
Pia amesema CRDB wamekua mstari wa mbele kuhakikisha wanawezesha wahitimu hao kwa kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe.
Ni mwaka wa 23 tokea kuanzishwa kwa taasisi ya AIESEC ambapo Taasisi hiyo ina matawi Katika nchi ziapatazo 110 ambayo Ina lengo la kuhakikisha vijana wanapata taaluma ya kuzitua fursa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.