Habari za Punde

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Awapongeza Makamishna wa Bodi ya Kemeshini ya Utalii Zanzibar

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Makamishna Wapya wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, mkutano huo uliofanyika leo 10-5-2023 katika ukumbi wa Wizara Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said amewapongeza Makamishna wapya wa bodi ya kamisheni ya Utalii Zanzibar, katika Kikao cha kuwaaga baadhi ya Makamishna waliomaliza muda, kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo iliopo kikwajuni - Zanzibar .

Akizungumza mara baada ya kikao hicho Mhe. Simai amesema kuwa Uteuzi wa Makamishna hao, Uliangalia zaidi Uzalendo ambao unaendana na kasi na Matarajio ambayo Mhe. Rais anataka .
Aidha katika Kumsaidia Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii na Kuishauri Wizara ya Utalii Zanzibar Mhe. Simai amewataka Wajumbe hao wa bodi kuja na Mitazamo, fikra na Mpango mkakati ambao Wizara inaweza kuitumia katika kuutangaza na kuendeleza Utalii wa Zanzibar.
Mhe. Simai amewataka Makamishna hao kuwa Wabunifu katika kuwahimiza na kuwashauri Wawekezaji kusaidia zaidi mambo ya kijamii ikiwemo Elimu, Afya na Maji jambo ambalo litasaidia sana kuboresha huduma ndani ya Sekta ya Utalii.
Waziri Simai amewaomba Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Kwa Ujumla kuendelea kuwa Mabalozi wazuri katika kuwaelekeza na kuwaongoza Wageni wanaofika Nchini .
Nae Mwenyekiti wa bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mhe. Rahim Bhaloo amesema kuwa Uzoefu, Ubunifu na Uzalendo pamoja na Mbinu mbadala walizonazo Makamishna hao zitasaidia kufanikisha na kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.






Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar, baada ya kumaliza mkutano wake na Makamishna hao uliofanyika katika ukumbi wa Wizara Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 10-5-2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.