Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Mei 29, 2023 ameongeza kikao cha Mawaziri wa nchi za Kenya na Uganda kwa njia ya mtandao ikiwa ni muendelezo wa vikao vya pamoja kwa nchi hizo kuandaa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027, ambacho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma.
Katika kikao hicho viongozi hao wameeleza utayari wa Wakuu wa nchi hizo na tayari Mashirikisho ya Mpira wa Miguu yote yamewasilisha andiko la kuomba kuandaa mashindano hayo kwa Wakuu hao wa nchi.
Vile vile, kimeazimia kuunda Kamati ambayo itaratibu maandalizi ya awali ya ukaguzi ambao utafanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa ajili ya kuangalia utayari wa nchi hizo kuweza kuandaa Michuano hiyo.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara Bw. Saidi Yakubu na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndg. Wallace Karia.
No comments:
Post a Comment