RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ikulu, Zanzibar.
Akipokea ripoti hiyo Rais
Dk. Mwinyi amemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na
Utawala Bora kuiwasilisha katika Baraza la Wawakilishi.
Akizungumza baada ya
kukabidhi riporti hiyo kwa Rais Dk. Mwinyi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) Dk. Othman Abass Ali CAG, alisema wamewasilisha ripoti saba
ikiwemo ya Serikali Kuu (Mawizara na taasisi zote), Mashirika na Taasisi
zinazojitegemea, ripoti ya Idara Maalum na taasisi zake, ripoti ya mifumo yote
ya Tehema ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ripoti ya mashirika ya Umma, na
ripoti ya ufanisi ya miradi ya Maendeleo iliyofadhiliwa na fedha za Uviko 19.
Alisema ripoti hizo
zipo za aina mbili ikiwemo miradi ya maendeleo ya wahisani pamoja na ya Serikali
pamoja na ripoti za kiufundi.
“Tunapojenga
tunatakiwa kufanya ukaguzi wa thamani ye fedha, tumefanya ukaguzi huu kwa sekta
za Afya na Elimu kwa skuli zote 12 zilizojengwa” alielza CAG.
Pia alieleza
walifanya ukaguzi kwa skuli ya Bweleo ambayo Serikali iliinunua na skuli zote
zilizofanyiwa matengenezo ikiwemo vyoo vya skuli hizo na kuonesha yote
yaliyobainika kwenye ukaguzi huo.
Kifungu cha 112 (5)
kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali awasilishe taarifa
yote aliyoikagua na aikabidhi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi kwa hatua nyengine.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment