Habari za Punde

Rais wac Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Awasili Windhoek nchini Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIC) tarehe 07 Mei, 2023. Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia kwa ajili ya mkutano wa Dharura wa TROIKA Plus utakaojadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Watoto Miranda Masatu wa kwanza kulia, pamoja na Samra Mdee mara baada ya kuwasili Windhoek, Namibia tarehe 07 Mei, 2023. Wa kwanza kulia ni Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob akishuhudia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.