Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na Viongozi mbalimali na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Harous Said Suleiman na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dk. Omar Dadi Shajak Katibu Mtendaji wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Ussi Khamis Debe, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wenye Ulemavu Salma Saadat Haji na Mkurugenzi wa Mpango wa Elimu ya Maandalizi Zanzibar Sharifa Majid.
IMEELEZWA kwamba Watu Wenye Ulemavu wanaendelea kukabiliana na changamoto kadhaa hapa Zanzibar ikiwemo kutengwa, kubaguliwa na hata kutendewa ukatili, licha ya jitihada kadhaa za serikali zinazoendelea kuchukuliwa kwa kushurikiana na Jumuiya mbali mbali zinazoshughulikia masuala ya watu wa jamii hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameyasema hayo hoteli ya Madinat
libahari Mbweni Zanzibar, alipofungua mafunzo
kwa viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Wakuu wa Wilaya na Mikoa, Makamanda
wa Polisi wa Mikoa na Wilaya kuhusu uzingatiaji wa masuala ya watu wenye
Ulemavu Zanzibar.
Mhe. Makamu amefahamisha
kwamba hatua hiyo inafuatia masuala ya watu wenye ulemavu kupewa
kipaumbele ulimwenguni kote baada ya
kubainika kundi hilo ambalo ni sehemu ya jamii kukosa haki zake za msingi na
kupelekea Umoja wa Mataifa kuanzisha Mkataba wa watu wenye ulemavu duniani.
Hivyo Mhe . Othman amesema katika kutekeleza
Mkataba huo serikali ya Mapinduzi Zanzibar imechukua jitihada mbali mbali za kuhakikisha watu wenye Ulemavu wanapata
haki na fusra mbali mbali wanazostahiki
ili waendelee kuishi vyema kama wengine wote.
Mhe. Makamu alizitaja miongoni mwa
jitihada hizo kuwa , pamoja na mambo mengine ni pamoja na kutungwa sera ya watu
wenye Ulemavu ya mwaka 2008 na kutungwa
kwa sheria mpya inayosimamia masuala mbali mbali ya Watu wenye ulemavu ya mwaka
2022 Zanzibar.
Hivyo Mhe. Makamu amewataka wakuu
wa wilaya za Zanzibar kwa kuzingatia
kifungu namba nane cha sheria hiyo kwa kuanzisha
na kuyasimaia Mabaraza ya Watu Wenye Ulemavu ndani ya wilaya zao ili
yaweze kufikia malengo ya kuwapa huduma bora watu wa jamii hiyo, sambamba na
kuwashajiisha masheha wote nchini kuwafichua na kuwasajili watu wenye ulemavu katika shehia zote hapa Zanzibar.
Aidha Mhe. Othman ametoa wito kwa
jamii yote nchini kuhakikisha kwamba
wanawapenda na kuwajali ipasavyo watu wenye ulemavu na kuacha kabisa tabia ya baadhi ya watu kuwadhalilisha pia kutowaita majina yasioyofaa kwa kuwa kila mmoja ni mlemavu mtarajiwa.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Dk. Omar Dadi Shajak, amesema kwamba mafunzo hayo ni
muendelezo na jitihada za Serikali
kupitia Ofisi hiyo katika kuifanya jamii na viongozi nchi kuwa na uwelewa mpana
kuhusu masuala yote ya watu wenye ulemavu nchini.
Katika mafunzo hayo ya siku moja mada mbali mbali zimewasiliwashwa na kujadiliwa ikiwemo dhana ya watu wenye ulemavu, uzingatiaji wa masuala ya watu wenye ulemavu , nyaraka za kitraifa na Kimataifa zinazohusu watu wenye ulemavu na sheria mpya ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akifungua mafunzo ya siku moja juu ya
uzingatiaji wa masuala ya watu wenye ulemavu Zanzibar leo tarehe 27.05.2023
huko katika Hoteli ya Madinat Libahar Mbweni Zanzibar kushoto kwa makamu ni
Mwenyekiti wa Baraza la watu wenye Ulemavu Zanzibar Bi Salama Saadat Haji. Mfunzo hayo yamewajumuisha watendaji wa
serikali za Mitaa wakiwemo wakuu wa
Wilaya na mikoa pamoja na Makamanda wa Polisi wa Wilaya na Mikoa kutoka Unguja
na Pemba. Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment