Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahudhuria Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa Wimbo wa Taifa ukiimbwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) tarehe 10 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea Jukwaa Kuu mara baada ya kukagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele wakati Gwaride la JKT likipita mbele ya Jukwaa Kuu wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
Gwaride la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likipita kwa mwendo wa pole na haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.