Habari za Punde

Bodi ya Wakurugenzi (DUWASA) Watembelea Mradi wa Maji Nzuguni Dodoma

MAFUNDI kutoka kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakiendelea na kazi ya kumwaga zege katika ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika Mradi wa maji wa Nzuguni jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo ya ramani kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph wakati bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo ilipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (kulia) akiwa na wajumbe wa bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkandarasi Noel Lukuwi kutoka Kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma
MAFUNDI kutoka kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakiendelea na kazi ya kumwaga zege katika ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika Mradi wa maji wa Nzuguni jijini Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (wanne kushoto) akiwa na wajumbe wa bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.