Habari za Punde

Ureno kuanza safari za moja kwa moja za kitalii Zanzibar


Ndege ya HIFly A-330 kutoka Lisbon, Ureno ikiwasili kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Abeid Aman Karume na kukaribishwa rasmi kwa maji baada ya kuwasili
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum akikata keki baada ya kuipokea rasmi kwa mara ya kwanza ndege ya HiFly kutoka Lisbon Ureno huku akishuhudiwa na Waziri a Utalii na mambo ya kale Zanzibar mhe Simai Mohammed Said
Wajumbe wa serikali wakiwemo mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kampuni Solérias na Sonhando baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza kwa ndege ya HIFly moja kwa moja kutoka Ureno

 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepokea ndege inayofanya Safari moja kwa moja kutoka Nchi ya Portugal ( Ureno) kuja Zanzibar kwa mara ya kwanza ikiwa ni katika kuimarisha Sekta ya Utalii Nchini.
Ndege hiyo aina ya HiFly A-330 iliyokua imebeba Watalii 288 imepokelewa na kuzinduliwa leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal 3 na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Khalid Salum .
Akizungumza mara baada ya Mapokezi hayo Mhe. Dkt. Khalid amesema kuwa awamu hii imekua tofauti na awamu nyengine ambazo hua zinapokelewa ndege kutoka nchi mbali mbali lakini awamu hii ni Serikali imetoka kwenda kutafuta ndege na hatimae kufanikisha kuileta nchini hii ni hatua kubwa mno.
Nae Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai Mohammed Said ameishukuru sana kampuni ya Solérias na Sonhando za nchini Portugal kwa ushirikiano walioonesha katika kufanikisha lengo linafikiwa.
Akiendelea na Shukrani zake Mhe. Simai amesema kwa Upekee kabisa Shukrani za dhati zimuendee Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa nguvu kubwa aliyowekeza kuiwezesha na kuielekeza Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kutafuta soko jipya katika sekta ya Utalii ili kuzidi kuongeza Idadi ya wageni nchini na kukuza pato la nchi.
Ndege ya HiFly itakua inakuja mara mbili kwa wiki na zinatarajiwa kua saba zenye madaraja tofauti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.