Habari za Punde

Usafiri wa Mabasi Mapya Umeanza Kutoka Afrika Kusini Hadi Tanzania. Sasa Unaweza Kusafiri Moja kwa Moja Kutoka Johannesburg Hadi Dar es Salaam

 

Na Mwandishi  Zainabu Hamis.
Habari njema na za kufurahisha kwa sasa watanzania wanaweza kusafiri kwa raha mustaree kwa usafiri wa basii kutoka Dar-Es-Salaam hadi Johannesburg, Afrika Kusini kwa kutumia mabasi mapya kabisa. ya kampuni ya kizalendo ya Kitanzania Mkombe Luxury Bus ambayo ina makao yake Johannesburg Afrika kusini.

Kampuni hiyo kitanzania imekuja na suluhisho la kurahisisha Safari za kutoka hapa nchini hadi Afrika kusini,kwa sasa wasafiri wa Tanzania na Afrika Kusini wanaweza kutumia usafiri huo wa Mkombe Luxury Bus ambao nauli yake ni
Tsh 350,000 za kitanzania kwa safari moja na wanaweza kulipia nauli ya Tsh,700,000(laki saba) kwenda na kurudi.

Kampuni hiyo imefungua ofisi zake mtaa wa Shekilango jijini Dar-es-salaam ambapo tiketi zinapatikana pia wanapatikana kwa whats app +27604749717 Wasafiri wa Tanzania na South Africa wanaweza kutumia usafiri kwa kupitia Zambia, maporomoko ya maji ya Victoria Falls, Zimbabwe hadi Johannesburg Afrika Kusini basi linachukua siku tatu hadi Afrika kusini,Kampuni hiyo ya kizalendo Mkombe imekuja kurahisisha ufasari wa kwenda na kurudi hadi Afrika Kusini na pia wana magari magari ya kusafirisha mizigo.

Safiri kwa Raha na Mkombe Luxury Bus ambayo ndani ya Choo,TV na WiFi ya internet safarini kote. Watanzania wanaposafiri na usafiri huu Luxury Mkombe Bus ni Utalii Tosha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.