Habari za Punde

Wizara ya Fedha Yashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Nane nane Jijini Mbeya

Mchumi, Idara ya Usimamizi wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Neema Msola (kushoto), akitoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo, kwa Bw. Michael Harsory (kulia), aliyetembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.

Mchumi, Idara ya Usimamizi wa Madeni, kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Wagana Kikerero (kulia), akitoa elimu kuhusu usimamizi wa deni la taifa, kwa Bw. Godlisten Mrema (kushoto), aliyetembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.
Mchumi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Msumule (kulia), akitoa elimu ya fedha, kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.
Mtaalamu wa masuala ya pensheni wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Gillian Makule (kulia), akitoa elimu kuhusu masuala ya pensheni inayotolewa na Wizara ya Fedha, kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.

Watumishi wa Kitengo cha Maktaba kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Tumaini Mtalemwa (kushoto) na Bi. Upendo Kavalambi (kulia), wakisikiliza kwa umakini maoni yalikuwa yanatolewa na Meneja waKampuni ya Bima ya Sanlam Life Kanda ya kusini Bw. Moses Mwakyelu, aliyetembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.

Mtaalamu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Wizara ya Fedha, Bw. Edwin Kachenje (kulia), akitoa elimu kuhusu masuala ya pensheni inayotolewa na Wizara ya Fedha, kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Kulia ni mtaalamu kutoka Kitengo hicho, Dkt. Aloyce Masanja

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF-Mbeya)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.