RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuyafanyia
kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Maboresho
ya mifumo ya taasisi za Haki jinai ambayo itatoa mwangaza kwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu kuboresha mifumo na
taasisi zinazohusiana na masuala hayo kwa nia ya kupatikana haki kwa ufanisi.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar
alipokutana na tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Mohamed Othman
Chande na Makamu Mwenyekiti Balozi Ombeni Sefue walipomkabidhi ripoti ya tume
hiyo.
Alieleza Serikali zote mbili ya Mapinduzi ya
Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeyapokea mapendekezo hayo na
kuahidi kuyafanyia kazi kwa kina ili kuleta mabadiliko na mageuzi makubwa kwa
nia ya kupatikana kwa haki nchini.
Alisema utekelezaji wa mapendekezo hayo kwa kiasi
kikubwa unaendana na kutegemeana na taasisi zote za haki jinai za Bara na Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi alizungumzia ushirikiano mzuri
uliopo baina ya taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa ya Zanzibar ZAECA na ya
kupambana na dawa za kulevya, zimepata msaada wa kujengewa uwezo na wenzao kutoka Bara kwa kupewa mafunzo.
“Bila shaka ni sahihi kabisa lazima kuwe na
kubadilishana ujuzi na uzoefu, ushirikiano wa karibu” alisifu Rais Dk. Mwinyi.
Kuhusu mahakama ya rufani kufanya kazi zake Zanzibar,
alisema tayari suala hilo linashughulikiwa pamoja na kuisifu Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa miundombinu ya Mahkama
kuu ya Zanzibar.
Naye, Mwenyekiti wa Tume
hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, alimueleza Dk. Mwinyi kwamba
tume ilifanikiwa kuzifanyia kazi changamoto za taasisi 15 zilizopendekezwa na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo Jeshi
la Polisi, Ofisi ya taifa ya Mashitaka, Jeshi la Magereza.
Taasisi nyengine ni Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa,
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Mahakama ya Tanzania, kitengo
cha kudhibirti fedha haramu Uhamiaji, Mkemea Mkuu wa Serikali na taasisi
nyengine zinazohusu masuala ya jinai kwa kutathmni ushirikiano wa taasisi hizo na kuangalia
nidhamu, mifumo ya ajira, viwango vya weledi, tume ya upandishaji vyeo, ufanisi
mahusiano, nidhamu, ufamnisi
matumizi ya teknolojia na motisha.
Tume ya maboresho ya mifumo ya taasisi za Haki jinai imeundwa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Januari 31 mwaka huu
na ilianza kazi zake mapema mwezi Februari kwa lengo la kutathmni mifumo ya
haki jinai na kutathmini taasisi za haki jinai.
No comments:
Post a Comment