Habari za Punde

Kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar

Mmoja katika washiriki wa  kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar akitoa mchango wake wakati wa kikao
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said akizungumza wakati alipokuwa akiifunga kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Ukumbi wa Golden Tulip Hotel


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema, ni muda sasa kwa kila mwalimu kuchukua hatua ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kupata matokeo mazuri zaidi.

Amesema hayo wakati wa kufunga kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Katika ukumbi wa mikutano Golden Tulip uwanja wa ndege Mjini Unguja.
Amesema, ili Walimu waendelee kufanya kazi kwa juhudi kubwa Wizara itaendelea kufanya kila namna kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Walimu nao wanaendelea kupewa Mafunzo ili kuendana na mabadiliko ya Teknolojia.
Amesema, Zanzibar ili iendelee kupata matokeo mazuri ipo haja ya kila muhisika kutimiza wajibu wake kwa kuengeza bidii zaidi.
Nao washiriki wa kikao hicho wamesema, Serikali inaendelea na jitihada kwa kuimarisha sekta ya Elimu kuanzia miundombinu hadi vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Hivyo ni vyema kwa kuzithamini bidii hizo ili taifa iendelee kupata matokeo mazuri zaidi.
Mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha viongozi mbalimbali wa Wizara ya Elimu Zanzibar, Wawakilishi kutoka KOICA, Wawakilishi kutoka good Neighbours na wadau mbalimbali wa Elimu nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.