Habari za Punde

*WAZIRI DKT. DAMAS NDUMBARO ASISITIZA UBUNIFU NA KASI YA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI *

 

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Septemba 6, 2023 Jijini Dodoma ameendelea kukutana na kuzungumza na Watumishi wa baadhi ya  Idara za Wizara hiyo kwa lengo la kufahamiana, kutambua majukumu wanayotekeleza na vipaumbele katika kuwahudumia wananchi.

Akizungumza wakati wa ukaribisho wa Waziri huyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nicholas Mkapa  amemueleza  Waziri, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  kuwa wizara hiyo inaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi pamoja na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Watumishi hao kutoka Idara ya Michezo amewasisitiza waongeze kasi ya utendaji, kushirikiana katika kazi pamoja na ubunifu kwa kuwa Idara hiyo imebeba jukumu kubwa la kutoa burudani kwa Watanzania kwa kuwa Sekta ya michezo inaajiri vijana wengi hivyo ni lazima iongeze ubunifu na mikakati katika utekekezaji wa majukumu yake.

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro  amezungumza pia na Watumishi wa Kitengo cha Uhasibu, Ukaguzi wa Ndani, Ununuzi na Ugavi pamoja na TEHAMA akisisitiza bidii, ubunifu na uwajibikaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.