Habari za Punde

Mhe.Katambi Ampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu kwa Kuyajali Makundi Maalumu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kulia) Septemba 6, 2023 akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alipo wasili katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi Septemba 6, 2023 akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini, wa pili kushoto ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa tatu kulia) Septemba 6, 2023   akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (wan ne kulia) katika Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini

Na. Mwandishi wetu – Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuyajali makundi maalum ya vijana, Watoto, wazee na wenye ulemavu.

Mhe. Patrobas Katambi amesema hayo Septemba 6, 2023 katika Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye amefungua Mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa hao kutoka Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na sekta binafsi zinazotoa huduma za ustawi wa jamii nchini..

Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa makundi hayo aliunda Wizara mahsusi kwa ajili kushughulikia masuala yanayohusu makundi hayo ikiwemo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu na Ofisi hiyo.

Aidha, amewasisitiza Maafisa Ustawi wa Jamii kutambua matatizo na changamoto zinazokabili makundi hayo na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto hizo kwa  kutumia rasilimali zilizopo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.