Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Equity Tanzania Isabella Maganga akiangalia hatua za utengenezaji wa sabuni ya maji kutoka kwa wanafunzi wa Skuli ya Trifonia Academy wakati aliposhiriki mahafali ya 15 na kumbukizi ya kutimiza mioaka 25 ya kuanzishwa kwa skuli hiyo huko Mambosasa Zanzibar.
Na Fauzia Mussa Maelezo
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bora kwa wanafunzi Benk ya Equity imesema itaendelea kusaidia huduma zinazohitajika ikiwemo vifaa vitakavyowezesha wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.
Akizungumza katika Mahafali ya 15 na Sherehe ya kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Skuli ya Trifonia Academy Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Equit Tanzania Isabella Maganga amesema hatua hiyo itawasaidia walimu kuwasomesha wanafunzi katika mazingira yaliobora ili kuongeza ufaulu mzuri kama ilivyo adhma ya Serikali .
Aidha aliwasisitiza wazazi na walezi kuwa tayari kuwapokea watoto wao, kwa kuwa nao karibu na kufuatilia nyendo zao ili kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji mara tu wanaporudi majumbani mwao.
Alisema malengo ya mtoto wa kike ni makubwa Sana hivyo ipo haja wazazi kushirikiana na walimu katika kuwaendeleza na kuhakikisha wanafikia malengo waliyoyatarajia.
Vilevile aliiwashauri Walimu kuwafundisha wanafunzi kazi za mikono za kujishughulisha wanaporudi katika jamii ili kuepuka kukaa katika vikundi viovu.
“Tujitahidi kuwafundisha kazi za amali na ujasiriamali ili wapate maarifa yatakayowasaidia baada ya kumaliza masomo na kuchanganyika na jamii”alisistiza Isabella
Hata hivyo Aliwataka mabinti kutokuuchezea muda ambao watakua wanasubiria hatua nyengne ya masomo na kuwataka kujiendeleza katika kazi za mikono ili wawe Wanawake wa mfano watakapoanza maisha ya uraiani
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Skuli yaTrifonia Grese Peter Myamba aliwasisitiza wanafunzi kujiandaa vyema na Mitihani yao ya Taifa na kuwashukuru wazazi na walezi kwa mashirikiano yao hadi kufikia kutimiza miaka 25.
Mapema akisoma risala ya wanafunzi Mwanafunzi Rauhiya Othman Ali amesema Skuli ya Trifonia imepata mafanikio mengi ikiwemo kuwa na mahusiano chanya kati yao na jamii.
Mbali na hayo alieleza kuwa skuli inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya kusomea kwa vitendo pamoja na vitabu vya ada na kiada.
Alifahamisha kuwa skuli hiyo ipo pembezoni mwa barabara finyu ,hivyo waliiomba Serikali kuongeza alama za barabarani,matuta na kuweka Askari wakuongoza wanafunzi wakati wa kwenda na kurudi Skuli ili kuepusha ajali za mara kwa mara.
Katika mahafali hayo jumla ya Wanafunzi 68 wa kidato cha nne, 74 wa darasa la saba walikabidhiwa vyeti vya kuhitimu.
Wahitimu wa Darasa la Saba Skuli ya Trifonia wakiimba wimbo maalum wakati wa sherehe ya mahafali ya 15 na kumbukizi ya kutimza mika 25 tangu kuanzishwa kwa skuli hiyo.
Muhitimu wa kidatu cha nne Skuli ya Trifonia Rauhiya Othman Ali akizoma Risala ya wanafunzi wakati wa sherehe ya mahafali ya 15 na kumbukizi ya kutimza mika 25 tangu kuanzishwa kwa skuli hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya Equity Tanzania Isabella akimkabidhi cheti muhitimu wa kidatu cha nne Awatif Malik wakati wa mahafali ya 15 na sherehe ya kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwa skuli hiyo huko Mambosasa Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment