Habari za Punde

Mfumko wa Bei za Chakula Wapanda

Mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za bei Salma Saleh Ali akiwasilisha ripoti ya Takwimu za bei  huko Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANIBAR

Na.Khadija Khamis –Maelezo .09/10/2023

Hali ya Mfumko wa bei ya bidhaa mbali mbali zimeongezeka kwa kipindi cha miezi 12 hadi kufikia mwezi wa septemba 2023  na  kufikia asilimia 7.45 kutoka asilimia 6.82.

 

Akiwasilisha takwimu hizo mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za bei Salma Saleh Ali amesema ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa katika kundi la  chakula na vinywaji visivyo na vileo kwa kwa asilimia 13.94.

 

Akieleezea baadhi ya bidhaa zilizopelekea kuongezeka kwa Mfumko wa bei kwa mwaka huu amesema ni pamoja na mchele wa mapembe kwa asilimia 37.58 ,mbeya asilimia 15.13,Unga wa ngano asilimia 3.88 Unga wa Sembe 11.02, Sukari nyekundu 29.87 nyeupe 27.3,

 

Akifahamisha  Mfumko wa bei za bidhaa za chakula wa mwaka unaoishia mwezi wa septembar mwaka huu umeongezeka na kufikia asilimia 14.39 ikilinganishwa na asilimia 12.04 iliyorikodiwa katika mwezi wa Agosti 2023.

 

Hata hivyo alisema kuwa mfumko wa bei ya bidhaa zisizo za chakula kwa mwaka umepungua  na kufikia asilimia 2.69 kwa mwezi wa Septemba 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.22 iliyorikodiwa katika mwezi wa agosti 2023. 

 

Mchumi Mwandamizi wa Benki kuu ya Tanzania ultrick Alieleza  kuwa ongezeko la  bei ya  bidhaa za chakula na sisizo za chakula  zimetokana na  kupanda kwa  bei ya mafuta  pamoja na uhaba wa  upatikanaji  wa dola.


Mfumko wa bei wa Zanzibar ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbali mbali zinazokusanywa katika masoko ya mji wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.