Habari za Punde

Maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Reli Kitaifa Kufanyika Tabora

Mkuu wa wilaya ya Uyui  Zakalia Mwansasu akizungumza  kwenye Maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli yanayofanyika kitaifa mkoani hapa kwenye uwanja wa chuo cha Teknolojia ya reli  .
Waendesha bodaboda waliopatiwa vyeti baada ya kupata mafunzo maalumu yaliendeshwa na jeshi la usalama barabara wakiwa katika picha ya pamoja na  Afisa Uhusiano Wa shirila la reli Tanzania na Zambia Tazara Regina Tarimo.
Mkuu wa wilaya ya Uyui  Zakalia Mwansasu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa LATRA,TRC TAZARA na jeshi la polisi na zima moto  .

Na Lucas Raphael,Tabora

Serikali imesema kwamba  itamvumilia wala kufumbia macho Mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo vya hujuma kwenye Miundombinu ya reli na kuhatarisha usalama atachukuliwa hatua kali.


Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani  katika hotba yake iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Uyui  Zakalia Mwansasu kwenye Maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli yanayofanyika kitaifa mkoani hapa kwenye uwanja wa chuo cha Teknolojia ya reli  .

 

Alisema kwamba kitendo cha kuhujumu ya  Miundombinu ya reli ni kuhatarisha usalama wa reli na abiri kiwemo mbali mbalimbali zinazosafirishwa na shirikal hilo nchini..

 

Zakalia Mwansasu alisema suala la usalama wa reli litaendelea kuwa la msingi na kupewa kipaumbele ambapo sheria ya TAZARA imeainisha jukumu la serikali kwenye kuchukua hatua za udhibiti na uhujunu wa miundombinu na huduma za reli.


Alisema kwamba ili usafiri wa reli unakuwa salama na wenye tija ,Serikali ilitunga sheria y reli no.10 ya 2017 ambayo imejikita katika usalama na ulinzi wa Miundombinu hiyo.


Alisema kwamba Sheria ya Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ya mwaka 1995 imeainisha jukumu la Serikali kwenye kuchukua hatua za udhibiti dhidi ya uharibifu na uhujumu wa Miundombinu na huduma za reli hapa Nchini.


Aidha Mkuu huyo wa Wilaya  alisema pamoja na sheria hizo ,Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi imeandaa na inatekeleza kanuni zaidi ya 12 ya kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za reli unakuwa salama na unazingatia kikamilifu masilahi mapana ya Kiuchumi.


Mwansasu alibainisha kwamba pamoja na jitihada hizo ,Serikali ya Tanzania ilianzisha mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini (LATRA) ambaye ndiye mdhibiti wa sekta ya usafiri wa reli hapa Nchini ikiwa na lengo la kuhakikisha sheria,kanuni na Taratibu za usalama na uchumi katika sekta ndogo zinazingatiwa.


Hata hivyo aliipongeza LATRA kwa hatua wanazochukuwa na kulieleke,a shirika la reli Tanzania (TRC) KUBORESHA mfumo wa Tiketi Mtandao kwa abiria wa tren ili wajikatie tiketi  zao wenyewe popote walipo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Shirika la reli Tanzania Masanja Kadogosa alisema kwamba shirika la reli Tanzania katika kipindi hichi linaendelea na kampeni ya uelewa kwa jamii kususani usalama na ulinzi kwa kukarabati njia ,Mabehewa na vichwa vya Treni na kiongeza uelewa kwa watumishi kwa kiwapeleka kwenye mafunzo mbalimbali vya nadharia na vitendo ndani na nje ya nchi.


Kadogosa alisema kwamba katika kampeni hiyo wananchi watakumbushwa kuwa usalama ni kitu cha kwanza matika usafiri wa reli ,hivyo wazingatie matumizi sahihi ya alama kwenye maeneo ya vivuko,hibadhi ya reli, Stephenie na maeneo ya Miradi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.