Habari za Punde

Rais Samia Suluhu Hassan awasili Lusaka kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa nchini Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa amesimama pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Zambia ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia tarehe 23 Oktoba, 2023. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakifurahia vikundi mbalimbali vya burudani mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 23 Oktoba, 2023. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwapungia mkono moja ya kikundi cha ngoma za asili cha  Zambia wakati wa mapokezi Rasmi katika  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lusaka tarehe 23 Oktoba, 2023.

 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.