Habari za Punde

UWT Mkoa wa Magharibi Kichama Yampongeza Dkt.Mwinyi kwa Utendaji Wake Katika Kipindi cha Miaka 3

Viongozi  wa UWT Mkoa wa Magharibi Kichama wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya habari na mawasiliano ya ziara ya Mwenyekiti wa UWT Tanzania,Marry Pius Chatanda inayotarajiwa kufanyika oktoba 29 mkoani humo.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR


Na Fauzia Mussa,    Maelezo 

Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania  Mkoa wa Magharibi kichama umempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutekeleza vyema ilani ya chama cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitatu.

 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi  Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT Mkoa wa Magharibi Mziwanda Ibrahim Abdalla amesema utekelezaji huo haukua wa maneno bali unaendelea kuonekana  kwa vitendo.

 

 Alisema  mambo aliyoyafanya Rais huyo  katika kipindi kifupi ni ya kupongezwa  na  kupigiwa mfano kutokana na  kupindukia malengo.

 

Aidha alisema katika kipindi cha miaka 3 ya Dkt Mwinyi Serikali imefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa Nchini ikiwa  ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya skuli za ghorofa, kuboreshwa kwa masoko,kuanzishwa kwa Hospitali za Wilaya na Mkoa zenye vifaa vinavyokidhi haja ya  matibabu kwa Wananchi pamoja na kuongezeka kwa  miundombinu ya barabara za ndani kwa kiwango cha lami.

 

"Yalikua mabati, sasa ndani ya mabati kumechomoza Spitali,maskuli na masoko"alifafanua Mjumbe huyo

 

Amesema  Umoja wa Wanawake Tanzania  (UWT ) utaendelea kuunga  mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi zinazoonekana waziwazi za kuwaletea maendeleo Wananchi wake na kuahidi kuwarejesha tena madarakani  ifikapo 2025.

 

"Tulikua tunaona tu gari zinapita juu,Mpaka Tanzania bara gari zinapita juu,sasa tunaenda kuona kwa macho yetu dalili zimeanza kuonekana Mwanakwerekwe pale"alisema Mjumbe huyo

 

Wakati huohuo Mjumbe huyo  alitumia fursa hiyo kuwaomba wanachama,na wapenzi wa chama cha mapinduzi kuhudhuria katika  mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29  mwaka huu  katika  viwanja  vya  Mzee Mgeni Mambosasa mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mwenyekiti wao Taifa  katika Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.