Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wahitimu wa Kidato cha Nne katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Oktoba 5, 2023. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni (kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, Upendo Wella (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annastazia Tutuba (kulia)
Na Happiness Shayo-Same
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameahidi kujenga kisima kikubwa cha maji katika
Shule ya Sekondari Kibacha Wilayani
Same, kwa lengo la kuendeleza kilimo cha mbogamboga na kuboresha lishe bora
shuleni hapo.
Ameyasema hayo leo Oktoba 5, 2023
katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne
katika Shule ya Sekondari
Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
"Nimeguswa na ujumbe wa igizo la Watoto
hawa kuhusu changamoto ya maji, naomba nitamke kuwa nitaijengea shule hii
Kisima kikubwa cha maji ambacho pia kitawezesha kuendeleza kilimo cha mboga
mboga na viazi lishe kwa ajili ya kuchangia lishe ya watoto wetu na hivyo
kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha suala la lishe shuleni linapewa
kipaumbele" Mhe. Kairuki amesisitiza.
Mhe. Kairuki amefafanua kuwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan ni sikivu na ilishaiona changamoto ya maji wilayani hapo
hivyo, ipo kwenye hatua nzuri ya ukamilishwaji hadi kufikia mwaka 2024 Wilaya
ya Same itakuwa na maji ya kutosha.
Aidha, ameipongeza Serikali kwa
kutoa fedha za miradi mbalimbali ya elimu
ili kuboresha sekta hiyo.
" Serikali kupitia Mradi wa
Lipa kulingana na matokeo imetoa shilingi Billioni 7.5 kwa ajili ya ujenzi wa
mabweni, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika Shule za Sekondari za
Kidato cha Tano na Sita kote nchini."
Ameongeza kuwa Serikali pia
imetoa shilingi Billioni 48 kujenga Shule za Wasichana za Bweni katika mikoa 16
Tanzania Bara na kupitia Mradi wa SEQUIP.
Katika hatua nyingine, Mhe.
Kairuki amewaasa vijana wanaohitimu
Kidato cha nne kuzingatia maadili ya
Mtanzania na kuzingatia masomo.
"Vijana mnaohitimu Kidato
cha Nne mwaka huu, mnapaswa kuelewa kuwa
wazazi wenu na Taifa lina matarajio makubwa kutoka kwenu. Mnapaswa kuweka
jitihada katika masomo yenu na kuwa na maadili mema kwa ajili ya ustawi wa
Taifa letu ma msijiingize katika maadili yanayofedhehesha utamaduni wetu
ikiwemo ushoga na mengineyo." Mhe. Kairuki amesema.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 5, 2023 ambapo ameahidi kuwajengea Kisima cha maji kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji shuleni hapo.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb)(hayupo pichani) akizungumza katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro yaliyofanyika Oktoba 5.
Baadhi ya wazazi , ndugu, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya shule hiyo yaliyofanyika Oktoba 5.
Baadhi ya washiriki wa mahafali ya saba ya Kidato cha Nne ya katika Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio katika mahafali hayo yaliyofanyika Oktoba 5, 2023.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Ngoka Manongi akitambulisha baadhi ya wageni walioshiriki Mahafali ya saba ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 3,2023. Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kidato cha Nne mwenye changamoto ya ulemavu wa miguu, Naomi Mathayo katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Oktoba 5, 2023.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi cheti Mhitimu wa Kidato cha Nne, Shabani Ibrahim katika mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Kibacha, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Oktoba 5, 2023. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibacha, Ngoka Manongi.
Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiangalia maonyesho ya kisayansi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibacha akiwa ameongozana na uongozi wa shule pamoja na uongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same, kabla ya mahafali ya 7 ya Kidato cha Nne ya Shule hiyo iliyopo, Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Oktoba 5, 2023.
No comments:
Post a Comment