Habari za Punde

ZHSF yawafikia wenye ulemavu

Afisa masoko mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Asha Kassim Biwi a akizungumza na watendaji wa umoja wa watu wenye ulemavu kuhusiana na dhana ya  mfuko huo huko  Kikwajuni Mjini Unguja.

Afisa masoko mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Asha Kassim  akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji umoja wa watu wenye ulemavu  Shaibu Abdalla mohammed karatasi yenye orodha ya Hospital zinatoa huduma kupitia mfuko huo.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahma Khamis Maelezo                    17/10/2023

Viongozi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar wametakiwa kufikisha ujumbe kwa watu wenye mahitaji maalumu juu ya dhana ya Mfuko wa Huduma za Afya ili kuwajengea uwelewa.

Akizungumza na watendaji wa Umoja huo huko Ofisini kwao Kikwajuni Welless  Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa vHuduma za Afya  Asha Kassim Biwi amesema watu weye mahitaji maalumu wana haki kama watu wengine hivyo kupatiwa elimu hiyo itawasaidia kufahamu dhana ya mfuko huo.

 Aidha amewashauri kutumia  mbinu zao mbalimbali wanazotumia  ili kufikisha ujumbe kwa watu wenye mahitaji maaalumu ili na wao wanufaike na mfuko huo kwa vile na wao wana haki ya kupata huduma bora za afya.

Amefahamisha kuwa katika hatua  za awali mfuko umeanza kutoa huduma kwa waajiriwa wa Serikali na watotoambapo mchangiaji na watoto wake wa kuwazaa   wameanza kupata huduma kupatia mfuko huo na baada ya kukamilika kuendelea  na  wafanyakazi wa Sekta binafsi

Hata hivyo Afisa huyo  amewataka Watumishi wa Umma  kuharakisha kukamilisha zoezi la usajili katika Mfuko huo  ili kuwapa nafasi makundi mengine ikiwemo makundi  maalum.

Nae Mkurugenzi Mtendaji  wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Shaibu Abdalla Moh’d ameushuku Uongozi wa Mfuko huo kwa  kufika kwao na kusema kuwa  watahakikisha kila mmoja uanapata taarifa hizo kwa njia moja ua nyengne kwani bila ya Afya hakuna maendeleo

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.