Habari za Punde

Kikao cha Kuangalia Utekelezaji wa Baraza la Jiji kutoka Julai -I-Septemba kwa Mwaka wa Fedha 2023- 2024

Mstahiki Meya wa Jiji La Zanzibar Mahamed Mahmoud akizungumza katika kikao cha 12 cha Madiwani ambacho kilipokea  na Kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Ofisi ya Baraza la Jiji na Kamati za Kudumu za Baraza la Jiji la Zanzibar na Masuala mengine mbalimbali ,Kikao kilicho fanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Michenzani Mall.

Na Sabiha Khamis ,    Maelezo.

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Mohamed Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Jiji, amewataka Watendaji na Wananchi kuendelea kushirikiana ili  kukabiliana na maafa yanayojitokeza katika kipindi cha  mvua.

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya utendaji kazi , huko Ofisini kwake Michenzani Mall, amesema kufanya hivyo kutasaidai kumarisha usafi wa Mji hasa katika Kipindi cha Mvua za Vuli zinzoendelea kunyesha.

Kufuatia chanagamoto zinazojitokeza katika kipindi cha mvua Mstahiki huyo aliwataka watendaji wa Baraza hilo kuendelea  kusafisha mitaro na kuondoa majaa yasiyo rasmini ili kuzuia  madhara yasiotokee kwa kasi zaidi.

“Endapo hatukufanya kazi ile ya kusafisha mitaro, kuondoa majaa yaiyokuwa sio rasmini basi maji yangelituathiri zaidi na hasara ingekuwa kubwa zaidi” alisema Mtahiki Meya.

Hata hivyo aliwapongeza madiwani, watendaji na taasisi zote zilizowajibika kuhakikisha kwamba inaisaidia Zanzibar hususani Mkoa wa Mjini Magharib kukabiliana na mvua zinazoendelea.

Awali Mstahiki Meya alitumia fursa hiyo kutoa  pole kufuatia kifo cha kijana aliejitolea kusaidia kuzibua mtaro kwa maslahi ya Wananchi na wote walioathiriw a na mvua hizo kwa  namna moja au nyengine.

Hata hivyo alisema Baraza hilo litaendelea kuwajibika ipasavyo ili kuiarisha Mji kuwa safi na salama.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Jiji Zanzibar Said Salmini Ufuzo akiwasilisha utekelezaji wa Baraza hilo alisema katika  kipindi cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba limefanikiwa kuanzisha programu ya  kuwajengea uwezo madiwani na watendaji, kuwalipa stahiki Madiwani na watendaji wa ofisi,  kutoa huduma za utendaji na utawala, kuzisimaia manispaa za jiji pamoja na kubuni na kuendeleza miradi ya maendeleo ya Baraza hilo.

Alielezea kuwa jumla ya watendaji thelethini  wakiwemo madiwani, watendaji wa manispaa wa Mjini wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi  yanayohusiana na mfumo wa ukusanyaji taka ili kuboresha usafi wa Mji.

Nao baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakiwasilisha utekelezaji wa kamati zao Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mazingira Abdul-latif Omar Haji alisema katika   kuhakikisha Mji wa Zanzibar unakuwa safi, jumla ya ndoo mia tano za kuhifadhia taka (dust bin) zimegaiwa katika maeneo mbali mbali ikiwemo vituo vya afya, maskulini, manispaa za jiji, madrasa pamoja na watendaji wa Baraza la jiji ili kuimarisha usafi nchini.

Pia kamati hiyo ilifanikiwa kukagua mitaro ya maji taka na majaa yasiyo rasmini ili kuweka mazingira bora kwa wananchi.

Kikao hicho kilijadili utekelezaji wa kazi za ofisis za baraza la jiji na kamati za kudumu za Baraza la jiji Zanzibar kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka iliyoanzia julai hadi septemba mwaka wa fedha 2023-2024.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.