Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko akizungumza mara baada ya kukagua jengo la Wizara ya Nishati katika Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma. Pamoja naye ni Katibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy Yonaz pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko leo amekagua
maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.
Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko alikuta ujenzi unaendelea ambao kwa sasa umefikia asilimia 69 ambapo Mkandarasi ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aidha ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu),
unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.
No comments:
Post a Comment