Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023 /2024 Ikiendelea Uwanja wa Amaan Complex Zanzibar Timu ya Yanga Imeishushia Kipogo cha Bao 5-0 Timu ya Jamhuri.

Mchezaji wa Timu ya Yanga na Jamhuri wakiwania mpira wakati wa mchezo9 wao wa Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, katika mchezo huo Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo dhidi ya Timu ya Jamhuri kwa bao 5-0

Yanga wameandika bao lao la kwanza katika dakika ya 10  na ya 17 ya  mchezo huo kupitia mchezaji wake Crispin Ngushi, baada ya dakika ya 22  Yanga wamefanikiwa kuandika bao la pili kupitia mchezaji wake Kibwana Shomari katika.

Timu ya Yanga imechukua muda mchache wa kipindi cha kwanza na kuweza kuandika bao la Tatu katika dakika ya 36 ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Ckement Mzize na mshambuliaji Skudu ameweza kuipatia timu yake bao tano  katika dakika ya 45 ya mchezo huo.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.