Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024 Ikiendelea Katika Uwanja wa Amaan Complex Zanzibar Kati ya Timu ya KVZ na Jamus Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao 1-1

Mchezaji wa Timu ya KVZ  akijaribu kumpita beki wa Timu ya Jamus, wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024, Mchezo uliofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-.1.

 Katika mchezo huo  Timu ya Jamus imeandika bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Yousif Mursa kwa mkwaju wa penenti katika dakika ya 45 ya mchezo huo.

Timu ya KVZ imefanikiwa kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo huo kupitia mchezaji wao Yussuf Mfaume ameipatia timu yake bao katika dakika ya 63 ya mchezo huo kipindi cha pili.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.