Habari za Punde

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi Alazwa Hospitali kwa Maradhi ya Kifua


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi  amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari. 

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali.

Abdullah Ali Mwinyi 

Msemaji wa Familia

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.