Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan azungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Norway (Storting) Svein Harberg Jijini Oslo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Norway (Storting) Svein Harberg mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Oslo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Norway (Storting) Svein Harberg katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Oslo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi za Bunge la Norway (Storting)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Norway (Storting) Svein Harberg katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Oslo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipeana mkono na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Norway (Storting) Svein Harberg mara baada ya mazungumzo katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Oslo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kuwasili katika eneo la Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kwa mwaka 2024 Shirika la Fedha Duniani (IMF) limesema kuwa Tanzania inatarajia kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani.

Rais Samia amesema hiyo ni fursa kwa wawekezaji wa Norway nchini Tanzania kwani pia ina mazingira mazuri ya kisiasa, kijiografia na kiuchumi.

Wakati akihutubia Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika jijini Oslo, Rais Samia amebainisha zipo kampuni kadhaa za Norway zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kisiasa Tanzania ina amani chini ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye kuzingatia tunu za utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.

Kwa upande wa kijiografia, Rais Samia amesema Tanzania inafaa kwa uwekezaji kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa manane ya Afrika inayopakana nayo.

Kiuchumi Tanzania ina sera nzuri na imara za kiuchumi na kifedha huku ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) ukirejea kwenye 5.2% kwa mwaka. Unatarajiwa kufikia zaidi ya 6% kwa mwaka ujao kama ilivyokuwa kabla ya COVID 19.

Rais Samia amesisitiza fursa tano za kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati

mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na usafirishaji.

Rais Samia ameanza ziara ya Kitaifa nchini Norway kwa muda wa siku mbili baada ya kutoka kwenye ziara ya Kihistoria huko Vatican ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.

 

Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.