Habari za Punde

Mwakilishi Mteule Sharif Ali Shariff Akiwasili Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa Ajili ya Kuapishwa leo

Mwakilishi Mteule wa Nafasi za Rais Mhe. Sharif Ali Sharif akiwasili katika viwanjas vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuapishwa kuwa Muwakilishi, baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Mwakilishi Mteule wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Sharif Ali Sharif akitinga viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Jijini Zanzibar leo 14-2-2024.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zunberi Ali Maulid akimuapisha Mhe.Sharif Ali Sharif kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, hafla hiyo ya uapisha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Baraza Chukwani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Jijini Zanzibar.
Mhe. Sharif Ali Sharif akiwa katika ukumbi wa mkutanmo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akifuatilia Kikao cha Baraza la Wawakilishi baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza. Kikao cha Baraza la Wawakilishi Kilichoaza leo 14-2-2024.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.