Habari za Punde

Sema na Tanga Wakoshwa na Uwekezaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Waahidi Kuwa Mabalozi

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati wa ziara ya Kundi la Sema na Tanga mara baada kumaliza ziara hiyo yenye lengo la kuona uwekezaji uliofanywa na Rais Samia Suluhu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Frank Shega na kulia ni Mwenyekiti wa Sema na Tanga 

Na Mwandishi Wetu, TANGA

Kundi la Sema na Tanga leo wamefanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku wakifurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji na kuimarisha huduma za Afya hapa nchini na kuhaidi kuwa mabalozi wa kuisemea vizuri.

Wametembelea na wamejionea uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kitengo cha dharura (EMD), kitengo cha uangalizi maalumu (ICU), Kitendo cha radiolojia (CT-scan), Kitengo cha uangalizi maalumu kwa watoto wachanga (NICU), Wodi ya upasuaji, Kitengo cha kusafisha figo (Dialysis Unit)

Akizungumza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Japhet Simeo alisema kwamba kundi hilo ambalo ni wadau wa maendeleo walialikwa ili kuweza kuona huduma nzuri ambazo zinatolewa katika Hospitali hiyo na wamethibitisha kuwa uwekezaji ni mkubwa sana na wengi wao walikuwa na picha tofauti na waliyokuwa nayo awali na hawakuamini kama Hospitali hiyo ingeweza kuwa na vifaa kama hivyo na watu wanatibiwa na kupona.

“Ambao waliokuwa na hisia za zamani kwa sasa zitafutika maana wengine wanaamini yale mambo ya miaka 10 iliyopita bado, kwa hiyo Sema na Tanga wanaenda kufuta hayo mambo kwenye fikra za wananchi na tunaamini mtakuwa mabalozi wazuri wa kulisemea hili”Alisema

Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea kuboresha huduma huku akiishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilivyosimamia kuhakikisha rasimali zinazoletwa zinasimamiwa kikamilifu akianza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na Katibu Tawala Pili Mnyema namna wanavyompa ushirikiano mkubwa na hivyo kufanya kazi kwa kujiamini

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Kundi la Sema na Tanga alisema wana haja ya kuja kukuunga mkono kama wadau wa maendeleo kutembelea kutokana kujionea maboresho ya huduma yaliyosaidia kuondoa makelele yaliyokuwa yakisikika.

Alisema wametembelea wameona maboresho makubwa ,vifaa mbalimbali, nyenzo nzuri za kisasa.“Tuwaheshimu madaktari na wauguzi hapa nchini na tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu maana tutakuwa tunawavunja moyo kama kuna mtu atawahujumu sisi tupo tayari kuwasemea na kusimamia na nyie”Alisema

“Tunamshukuru Waziri Ummy kwa kuteletea Mganga Mfawidhi Mpya Dkt Frank Shega na zile kelele zilizokuwepo kwa sasa hazipo zimeondoka ameonyesha waledi mkubwa, tutakutetea kwa kazi yako nzuri unayoifanya bila kupepesa macho”Alisema.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Frank Shega akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Kundi la Sema na Tanga kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.