Habari za Punde

Tumuenzi Hayati Edward Lowassa Kwa Uzalenzo na Uwajibikaji Wake - Dk. Mwinyi

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema namna  bora ya kumuenzi Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipotoa salamu za pole na kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe:13 Februari 2024.

Aidha,  Rais Dk.Mwinyi ametoa salamu za Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan na wananchi wote kwa msiba huu. 

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa amejifunza mengi kutoka kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele  maslahi ya nchi.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.