Na.Mwandishi Wetu
Meya wa Jiji la Zanzibar Mhe. Mahmoud Mohammed Mussa amesema hali halisi ya utoaji wa huduma za ustawi wa jamii hivi sasa Zanzibar imepiga hatua nzuri kutokana na juhudi kubwa zilizoofanywa na Marais Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Mhe Mahmoud ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Maasfisa Ustawi wa Jamii wa Sekta ya Afya na Hospitali, katika ukumbi wa Kwa wazee Sebleni mjini Unguja, ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra za kuadhimisha siku ya Ustawi wa Jamii Duniani.
Amesema kutokana na juhudi hizo, jamii inapaswa kuwapongeza viongozi hao pamoja na kuwaunga mkono kutokana na jitohada hizo katika kustawisha vizuri maisha ya wazanzibari na Tanzania kwa ujumla.
Amesema ni imani yake ni kuwa mafunzo hayo yamefanyika vizuri na washiriki watayatumia vizuri kwa faida yao na wazanzibari kwa ujumla huku akiwapongeza kwa muitikio mzuri katika kupata elimu hiyo.
Akiwasilisha mada juu ya masuala ya Ustawi wa Jamii Meneja wa Wataalamu wa Ustawi Jamii katika sekta ya Afya, Hospitalini na kwenye vituo vya Afya katika jiji la Manchester UNITED KINGDOM, bibi Nanyorry Mwasha amesema, ameona kuwa Maafisa ustawi wa jamii wa Zanzibar wanafanya kazi katika mazingira magumu sana na wengine pia hawakubaliki katika jamii wala katika Taasisi, hivyo amewataka kutovunjika moyo huku akiendelea kuwasaidia katika kutoa elimu ili jamii na viongozi wajue umuhimu wao.
Amesema wameona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kutokana na Rais kufungua milango katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kuona nao kutoa elimu namna gani wataweza kufanya kazi katika jamii iliyowazunguka na kuendeleza ukuaji wa uchumi wa nchi.
Hata hivyo amewataka kuendelea kujifunza kupitia elimu masafa au mafunzo ya muda mfupi na mitandao mbalimbali kwa kujiongezea elimu ili waweze kuwa maafisa bora wa ustawi wa jamii chini na duniani.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kumekuwepo tatizo kubwa katika baadhi ya Taasisi ambapo waajiri wamekuwa wakiwapangia kazi kinyume na taaluma yao waliyosomea huku wakipewa vitisho kwa kufukuzwa kazi endapo hawatofanya kazi hizo, hali ambayo inadumaza taaluma yao.
Zainab Abdalla Kitole Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya na Abdulhamid Masoud Suleiman wamesema katika sehemu zao za kazi hawapewi kipaumbele kufanya kazi zao kama zinazowahusu kama inavyotakiwa.
Wamesema maafisa ustawi wa Jamii pia wanatakiwa kutoka na kutafuta changamoto na sio kukaaa oficni kwani kwenye jamii watu wana matatizo mengi na wanahitaji kusaidiwa.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maafisa Ustawi wa Jamii Zanzibar ZASWA, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Zanzibar yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa Ustawi wa jamii wanaofanya kazi katika Hospitali na sekta ya afya kwa ujumla pamoja na kutoa mashirikiano mazuri kwa maafisa Ustawi wa Jamii.
No comments:
Post a Comment