Habari za Punde

TAMWA Zanzibar Yafanya Tathimini Tuzo za Takwimu Kuhusu Wanawake na Uongozi Zilizotolewa Hivi Karibuni

Mkurugenzi chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA  Zanzibar Dkt. Mzuri Issa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa majumuisho ya tuzo za umahiri kwa waandishi wahabari za takwimu kuhusu wanawake na uongozi huko Ofisi za TAMWA  Tunguu Zanzibar.

Na Fauzia Mussa. Maelezo.14.03.2024.

Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Ofisi ya Zanzibar Dkt.Mzuri Issa amewataka wahariri kushirikiana na waandishi wao ili kushinda tuzo mbalimbali  zinazoshindaniwa.

 

Wito huo ameutoa katika Ofisi za TAMWA  Tunguu wakati wa majumuisho ya hafla ya tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari za takwimu kuhusu wanawake na uongozi zilizotolewa hivi karibuni.

 

Amesema endapo  wahariri watasimamia vyema waandishi hao wanapoandika  kazi hizo kutasaidia kukidhi vigezo vya tuzo hizo kutokana na uzoefu wao.

 

Amesema katika shindano hilo muitiko wa washiriki wa makala za Televisheni ni mdogo jambo ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa ila kuweza kuongeza idadi ya washiriki katika kipengele hicho.

 

Hata hivyo ameeleza kuwa majaji waliosimamia kazi hizo walifanya kazi yao kwa usawa, uadilifu na usiri huku wakizingatia ubora,weledi,ubunifu na mpangilio wa mada hadi kupatikana mshindi wa uhakika.

 

“Ushindi kwa waliofanikiwa haukuja kwa upendeleo bali ni kwa kukidhi vigezo.” Alieleza Dkt.  Mzuri

 

Dkt.Mzuri ameahidi kuwa Tamwa itaendelea kutafuta rasilimali fedha ili kuimarisha shindano hilo lenye lengo la kuinua sekta ya habari kwa kukuza vipaji vya waandishi na kuwajengea uwezo.

 

kwa upande wake Mkuu wa Majaji katika Shindano hilo Dkt. Abdalla Mohammed Juma amesema kwa mwaka 2023 washiriki wameongezeka ukilinganisha na mwaka uliopita na kuwaomba washiriki hasa wa makala za televisheni kuzingatia vigezo na masharti  ili kuweza kupata washindi wa kipengele hicho badala ya kupata washiriki pekee.

 

Vilevile amewashauri waandishi wa habari kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kufanya kazi zao za kila siku kwa uweledi kwani kazi hizo wanaweza kuzitumia pale tuzo zinapotangazwa.

 

“si vyema kusubiri tuzo inatangazwa ndio tunaanza kuifanyia kazi ,kazi zetu tunazofanya kila siku tunaweza kuzitumia kuzishindania  ikiwa tumezifanya vizuri  na  kukidhi vigenzo vya ushindani wa tunzo hizo” alisema Dkt.Abdalla .

 

Mapema Dkt Abdalla aliishukuru TAMWA na Wadau wao PEGAO na ZAFELA kwa kuwaamini na kuwapa jukumu la kusimamia zoezi hilo ambalo lilikamilika vyema .

 

Nao Baadhi ya washiriki akiwemo, Rehema Juma Mema wamewaomba washiriki wazoefu kuwapatia miongozo Waandishi wachanga ili nao waweze kushiriki na kufikia malengo yaliokusudiwa.

 

Hata hivyo wamewaomba Wadau kuiunga mkono Tamwa kwa ufadhili ili iweze kuandaa tuzo hizo mara kwa mara na kuwajengea uwezo waandishi juu ya masuala mbalimbali ikiwemo ya wanawake na uongozi.

 

Zaidi ya kazi 500 ziliwasilishwa kati ya hizo Makala 379 ni za Wanawake zikiwa katika  vipengele vya Redio, Magazeti, Televisheni na mitandao ya kijamii.

 Mkuu wa Majaji Tuzo za Umahiri kwa waandishi wahabari za takwimu kuhusu wanawake na uongozi  Dkt. Abdalla Mohammed Juma akizungumza kuhusiana na tuzo hizo  wakati wa majumuisho yaliyofanyika Ofisi za TAMWA  T unguu Zanzibar.

Jaji wa tuzo za umahiri kwa waandishi wahabari za takwimu kuhusu wanawake na uongozi Nasra Mohammed Juma akichangia katika majumuisho ya tuzo hizo yaliyofanyika Ofisi za TAMWA  Tunguu Zanzibar.

Mwandishi wa habari wa kujitegemea Salum Vuai akiuliza maswali kwa viongozi na waratibu wa tuzo za umahiri kwa waandishi wahabari za takwimu kuhusu wanawake na uongozi katika majumuisho ya tuzo hizo yaliyofanyika Ofisi za TAMWA  T unguu Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.