Habari za Punde

Waziri Mkuu kufanya ziara Mlimba kutembelea maeneo yaliyokumbwa na Mafuriko

Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara huko Halmashauri  ya Mlimba Mkoani Morogoro.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Mlimba kujitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anatarajia kufanya ziara kujionea maeneo yaliyoathirika na mvua.

Wito huo ameutoa katika Mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Mlimba leo tarehe 15/04/2024 ambapo amewaomba wananchi kujitokeza mapema  kwa wingi tarehe 16/04/2024.

Waziri Mkuu atapata nafasi ya kuwapa pole wenzetu waliokumbwa na mafuriko ya mvua na tutapata wasaa wa kuwasilisha taarifa zetu.

“Nishukuru Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kusaidia kuokoa watu kama mnavyofahamu kutokana na mafuriko ya hayo ya mvua, treni ya Udzungwa iliyokuwa na watu ilizuiwa kufika Mlimba lakini jeshi letu la Tanzania lilisaidia kuwaokoa watu na hakukutokea madhara yoyote” alisema Mkuu wa wilaya

Aidha serikali ilisaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua kupata chakula cha msaada ambacho kililetwa na helikopta.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.