Habari za Punde

Zanzibar Yazindua Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde (SAZI)

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akisisitiza jambo wakati  akizindua Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde(SAZI) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.

Na Ali Issa --Maelezo Zanzibar 13/4/2024

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema amepata Imani kubwa kuona kamati ya michezo alioiteuwa italeta matumaini makubwa katika sekta ya michezo Zanzibar kwani ina viongozi weledi wanao fahamu michezo kiuhalisia.


Ameyasema leo huko ofisini kwake migombani wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo ya SAZI Saidia Zanzibar ishinde.


Amesema bila shaka amefarijika na hatokuwa na hofu kwani wajumbe hao ni watu watendaji wazalendo ambao wanaimani kubwa na nchi yao.


Aidha aliwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa kumsaidia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi ili kuthamini juhudi zake anazo zichukuwa kuinuwa sekta ya michezo hapa Zanzibar na kuona kuwa inapiga hatua kubwa mbele na kupata ushindi wakati wa mashindano ya mpira wa miguu na michezo mengine.


Amesema wajumbe watumie wakati wao kufanya kazi kwa pamoja ili masilahi yalio kusudiwa yafikiwe kwa uwepesi zaidi.


Nae Mwenyekiti wakamati hiyo Mkuu wa MKoa kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahamud alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada anazo chukuwa kuimarisha michezo Zanzibar.


Aidha alimshukuru Waziri Tabia kwa heshima kubwa aliompa yeye na wajumbe wa kamati kwa kuteuliwa ili kuiletea mabadiliko ya kimichezo Zanzibar na kuahidi kamwe hatomwangusha.


Aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa na ushirikiano kwani mafanikio yoyote hupatikana kwa kuwepo ushirikiano madhubuti baada ya kuaminiana kufanya kazi kwa weledi mkubwa.


Aidha alimpongeza Rais kwa kazi kubwa anayo ifanya kwa Zanzibar katika sekta ya michezo na mamlaka nyengine katika mihimili ya nchi na kusema kuwa yeye binafsi ameshuhudia miundo mbinu mikubwa ipo ya michezo ilofanywa na Rais kwa kukarabati au ujenzi mpya wa viwanja vya michezao jambo ambalo apongezwe kwa jitihada zake kuthamini michezo Zanzibar.


Hata hivyo Ayoub alisema kuwa anasamini sekta ya michezo hapa Zanzibar kwani michezo ndio ilioleta vuguvgu kuipatia uhuru Zanzibar sekta ambayo imeaza mbali kihistoria.


Aidha alisema yeye binafsi kuwa kuna mategemeo makubwa ya tapatikana baada ya kamati hiyo kufanya kazi kwani mna watu weledi wenye uzoefu na uwelewa wakiwemo watu michezo watu wa Uchumi, kutoka benki,wafanya biashara,na waheshimiwa kutoka barza la wakilishi na watu wenye uzofu.


Alitoa wito kwa wadau kuijenga zanzibar kimchezo ili kupata mafanikio jambo ambalo linawezekana kwani weziwao Tanzania bara wanatumia frusa hiyo na mafanikioa yanaonekana.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita katikati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde(SAZI)iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamadi Rajab akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika hasfla ya Uzinduzi wa Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde(SAZI)iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa neno la shukurani baada ya  Uzinduzi wa Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde(SAZI)iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita katikati akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde(SAZI)baada ya kuizindua hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Migombani Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.13/04/2024.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.