Habari za Punde

Masheha Watakiwa Kuongeza Idadi ya Wanawake katika Kamati Zao

                                    

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abasi Ali  akizungumza na masheha katika kikao cha kuhamasisha kuanzishwa majukwaa ya wanawake kilichofanyika  Wilaya ya Mjini huko Amani katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini.

 Naibu Katibu wa Masheha Wilaya ya Mjini ambae pia ni Sheha wa Urusi Yussuf Juma Mtumwa akizungumza katika kikao cha kuhamasisha kuanzishwa majukwaa ya wanawake kilichofanyika  Wilaya ya Mjini huko Amani katika Ofisi ya Mkuu  Wilaya ya Mjini.


Baadhi ya Masheha wa Wilaya ya Mjini wakiwa katika kikao cha kuhamasisha kuanzishwa majukwaa ya wanawake kilichofanyika  Wilaya ya Mjini huko Amani katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini.

NA MPIGA PICHA WETU.

Na Ibrahim Dunia. Maelezo. 30.05.2024.                                                                                                               

Masheha nchini wameshauriwa kuongeza Idadi ya Wanawake katika kamati zao ili kuweza kupata uwiano wa kijinsia.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya jamii, jinsia na Watoto Siti Abasi Ali wakati alipokuwa akizungumza na masheha wa Wilaya ya Mjini huko Amani katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini.
Amesema kufanya hivyo kutasaidia wanawake kuwa na idadi kubwa katika uongozi sambamba na kuwarahisishia kueleleza matatizo yao na kupewa ushauri unaofaa.
‘‘Mwanamke mara nyingi hutaka kuzungumza tatizo lake kwa mwanamke mwenziwe anapopatwa hasa anapopata udhalilishaji kwenda kwa mwanamme kumwambia mwanamme anaweza kulichukulia swali hilo kawaida tu lakini anapokwenda kwa mwanamke mwenziwe inakua ni rahisi kusikilizwa’’ amesema Mkurugenzi huyo.
Aidha amewataka Waratibu wa masuala ya jinsia katika shehia kushirikiana na masheha katika kufanya usajili wa vikundi vyote vya wanawake vilivyosajiliwa na visivyosajiliwa ili waweze kuanzisha majukwa ya wanawake katika shehia zao.
Amesema kuwa kupitia majukwaa hayo yatawasaidia wanawake kupaza sauti na kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Nae Naibu Katibu wa Masheha Wilaya ya Mjini ambae pia ni Sheha wa Urusi Yussuf Juma Mtumwa amesema ipo haja ya kuwapatia elimu wanawake hao kwani baadhi yao wapo nyuma katika maswala hayo,elimu ambayo itawapa mwamko wa kujitokeza kujiunga na vikundi hivyo.
Nao masheha hao wameahidi kuyatekeleza yote waliopewa ikiwemo kuongeza idadi ya wanawake katika kamati zao ili kuweka uwiano sawa na kumuomba kuzidi kutoa elimu na kufanya ziara za mara kwa mara ili kuweza kuangalia utekelezaji wa maagizo anayoyatoa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.