Habari za Punde

Waziri Mhe.Haroun Azungumza na Vyombo vya Habari Kuhusiana na Wili ya Msaada wa Kisheria Zanzibar

Waziri wa Nchi OR Katiba,Sheria,Utumishi na Utawah Bora  Mhe.Haroun Ali Sleiman akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya tano ya wiki ya wiki ya msaada wa kisheria yanayotarakiwa Kufanyika juni 28 katika Ukumbi  wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Wilaya ya  Mjini.

Picha na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar. 



Na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya tano ya wiki ya msaada wa kisheria ifikapo Juni 28 , mwaka huu.

Akizungumza  na waandishi wa habari kuhusiana na wiki hiyo huko Mazizini Waziri wa Nchi OR Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora  Mhe.Haroun Ali Sleiman amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika    katika Ukumbi wa sheikh Idrissa Abdul wakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini na kuhudhuriwa na  wadau mbalimbali  wakiwemo viongozi  na watendaji wa Serikali ,Taasisi binafsi ikiwemo  Shirika la legal Services Facility (LSF),  Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), UNICEF, UN WOMEN pamoja na watoa na wataka huduma za msaada wa kisheria.

Ameeleza kuwa katika  maadhimisho hayo namba maalum ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi itazinduliwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma  hiyo  ndani ya jamii.

Aidha amesema katika kutambua mchango wa wasaidizi  wa kisheria tuzo za mwaka  za kitaifa za watoaji wa msaada wa kisheria kwa  Zanzibar zitatolewa katika maadhimisho hayo.

Mbali na hayo amesema wiki hiyo   itajumuisha shughuli mbalimbali  hadi kufikia kilele chake ikiwemo kampeni ya vyombo vya habari kuhusu wiki ya msaada wa kisheria,kongamano la vyuo vikuu kuhusu masuala ya msaada wa kisheria, kongamano la malezi ambalo litahusisha ujengaji wa kiimani na utoaji wa Elimu ya ushauri nasihi pamoja na utoaji wa huduma za msaada wa kisheria Unguja na Pemba.

Takribani washiriki  300 wanatarajiwa kuhudhuria katika maadhimisho ya siku hiyo yaliyoratibiwa na Idara ya Katiba na msaada wa kisheria kwa kushirikiana na LSF na UNDP yakiwa na  kauli mbiu "TUMIA TEKNOLOJIA KURAHISISHA UPATIKANAJI WA HAKI"

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.