Habari za Punde

Waziri Mhagama, akabidhi vifaa tiba Kituo cha Afya Liganga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akikabidhi vifaa tiba kwenye mkutano wa hadhara kwa ajili ya kituo cha afya cha Liganga katika ziara yake iliyofanyika kwenye kijiji hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akizungumza na wananchi katika Mkutano wake katika kijiji cha  Liganga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake walipotembelea katika shule ya msingi Mbolongo kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imejipanga kuboresha huduma za afya ili kuokoa vifo vya wakinamama na watoto wakati wa uzazi.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 09/07/2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Liganga iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri amesema, “kituo cha afya Liganga kimepata vifaa tiba vienye thamani ya shilingi Milioni mia tatu na hivyo kusaidia kuanza kutoa huduma za mabara na kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.”

 Ameelekeza wataalamu kuhakikisha wanaratibu vyema mipango ya kuunganisha kituo hicho na nishati ya umeme ambayo inatarajiwa kuunganishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa saba.

Waziri Mhagama ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na  kuhakikisha  zinafanya kazi vizuri.

Awali Dkt. Rashid Mfaume Mkurugenzi wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI amemshukuru Waziri Mhagama kwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Peramiho.

“Jitihada za Mbunge kuomba vituo vya afya vifaa tiba na hospitali zimesaidia sana kuboresha huduma za afya jimbo la Peramiho ambapo kwa mwaka uliopita wa fedha nyingi zilikuja Halmashauri ya Wilaya ya Songea,” alisema Dkt. Mfaume

Waziri anapambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya, na hizi ni jitihada kubwa ambazo zinapaswa kupongezwa.

Ameongeza kusema, zoezi la kukabidhi vifaa tiba ni ishara tosha  kwamba kituo cha afya Liganga kitatoa huduma zote zinazopaswa kuwepo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.