BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Maulamaa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia Waumini, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Shura Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2024.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk, Hussein Ali Mwinyi ameinasihi
jamii kuweka mkazo kwenye malezi ya vijana na watoto ili
kuwanusuru na mmomonyoko wa maadili.
Alhaj Dk, Mwinyi ametoa
tamko hilo leo tarehe 23 Agosti 2024 wakati akitoa salamu baada ya kujumuika pamoja
na waumini wa Kiislam kwenye sala ya Ijumaa, Msikiti
Shuraa uliopo Magomeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameeleza kumekuwa na
mmonyoko mkubwa wa maadili na vitendo viovu vinavyosababishwa na vijana wanaojihusisha
na matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe uliokithiri.
Amewahimiza wazazi kuhakikisha vijana
wanapata elimu ya dini kwa ajili ya kujitambua na kujiepusha na vitendo viovu.
Alhaj Dk, Mwinyi
amefahamisha Zanzibar ilikuwa nchi yenye sifa na kusimamia
maadili lakini yameporomoka kutokana na matumizi ya dawa za
kulevya kwa kundi kubwa la vijana.
Aidha, amewahimiza viongozi
wa dini kuendelea kuhubiri na kuwahimiza waumini kufuata misingi ya
dini ili kuirejesha nchi katika maadili mema.
Mapema Katibu Mtendaji
wa Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amewashauri
Watumiaji wa vileo kufikiria madhara ya mihadarati wanayotumia badala ya
kufikiria starehe ya muda mfupi.
Sheikh Khalid amesema,
dini ya kiislamu imekataza matumizi ya pombe kwa kufahamu athari zake kwa
mtumiaji na jamii na kusisitiza kwa vijana kurudi katika misingi ya
dini ili kujinusuru.
No comments:
Post a Comment