Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar limekanusha taarifa za Kutekwa kwa watoto visiwani Zanzibar na linamshikilia Habibu Rashid Omar (35) mkaazi wa Mwera ambae anatuhumiwa kuchapisha taarifa ya uongo kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kutekwa kwa watoto wanne huko Skuli ya Regezamwendo, hali iliyoleta taharuki kwa jamii.
Akizungumza na waandishi wa
Habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera amesema Zanzibar
ni salama na hakuna tukio lolote la utekwaji wa watoto na kwamba amewataka
wananchi kuzipuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa kupitia mitandao ya
kijamii.
Aidha DCP Chembera amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na Tukio hilo na linatarajia kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment