Habari za Punde

Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Amejumuika na Wanancxhi Katika Ibada ya Sala ya Ijumaa Masjidi Mwitani Chasasa Wete Pemba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia Waumini wa Masjid Mwitani Chasasa Wete Pemba, akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 1-11-2024.

Waumini wa Dini ya Kiislam Wete Pemba wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza na kuwasalimia,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijuma iliyofanyika katika Masjid Mwitani Chasasa Wete Pemba leo 1-11-2024.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha wanawapatia vijana wao elimu iliyo bora ili kuweza kupata wataalamu waliobobea katika fani mbali mbali na wenye hofu ya Mwenyezi Mungu.

 

Alhajj Hemed ameyasema hayo alipokuwa akiwasalimia Waumini wa Masjid MWITANI CHASASA WETE  PEMBA mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 

Amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. HUSSEIN ALI MWINYI inahitaji wataalamu waliobobea kwa kila fani ili kuweza kufanikisha malengo ya Serikali ikiwemo usimamizi nzuri wa miradi ya kimaendeleo.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni lazima kwa kila mzazi na mlezi kuhakikisha anawasimamia vijana wake katika kupata elimu zote mbili zitakazowasaidia  kukuwa kimaadili na kifikra sambamba na kuhakikisha wanafanya kazi kwa hofu ya kumuogopa Mweneyezi Mungu.

 

Alhajj Hemed amesema kuwa  Taasisi zote za Serikli na za binafsi zinahitaji wataalamu waliobobea watakao leta  ufanisi nzuri wa kazi, hivyo ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kumpatia kijana wake elimu ili kumuwekea msingi nzuri wa kimaisha.

 

 

Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla  kuendelea kuitunza Amani na utulivu uliopo nchini ili kuweza kuisaidia Serikali kufanya mambo ya maendeleo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

 

Amesema nchi yoyote ile duniani inahitaji amani na utulivu kwa wananchi wake ili iweze kupiga hatu za kimaendeleo hivyo kila wananchi anayo haki na wajibu wa kulinda na kuisimamia vyema amani kwa maslahi mapana ya nchi.

 

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa kila muumini kuweza kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wajane, mayatima na walemavu ili kuweza kupata fadhila kutoka kwa Allah ( S.W ) na akufikia malengo ya kuumbwa kwao.

 

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh ALI HILALI ALI amewataka waumini wa dini ya Kiislam kuishi kwa kufanya matendo mema ambayo yanamfurahisha Allah na kujua kuwa maisha ya hapa duniani ni Mapito tu.

 

Amesema kuwa uislamu umeweka utaratibu maalum katika kufanya kila jambo hasa lile la ibada hivyo ni wajibu wa  kila Muumini kufanya amali njema  zinazompendeza Mwenyezi Mungu  ili kujiandalia maisha yaliyobora mbele ya Allah.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe..01.11.2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.