Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wazanzibari kwa ujumla wametakiwa kuendelea kuidumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo nchini ili kuweza kuisaidia serikali kupiga hatua kimaendeleo.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid KWAMTUNGO uliopo SEBLENI mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema Nchi yoyote ile duniani ili iwe na maendeleo ni lazima kuwepo kwa amani na utulivu kwa wananchi hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuendelea kuitunza tunu ya amani iliyopo ambayo imeasisiswa na waasisi wa Taifa hili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni wajibu wa viongozi wa dini, siasa na jamii kuhubiri amani kwa wafuasi wake ili iendelee kudumu kwa maslahi mapana ya vizazi vya sasa na baadae.
Alhajj Hemed amewataka wazazi na walezi kukaa pamoja na vijana wao na kuhakikisha kuwa kila mmoja anatimiza wajibu wake matika kuitunza tunu ya amani iliopo nchini.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kipaombele cha Serikali ni kuhakikisha kuwa inasimamia amani nausalama ndani ya nchi hvy wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali kuu katika kusimamia amani na utulivu kwa wananch
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh ALI TWALIB amesema kuwa Dini ya Kiislam imewataka waumini kushikamana na kusaidiana kwa kila hali pamoja na kuamrishana kufanya mema na kukatazana mabaya ili kufikia malengo ya kuumbwa kwao hapa duniani.
Amesema kuwa kusaidiana na kuhurumiana huongeza mapenzi baina yao na kupelekea kufika malengo ya ucha mungu na kuwasisitiza waumini hao kufanya yale yote ambayo yameamrisha na Mwemyezi mungu na kuacha yale yote ambayo yamekatazwa ili kufikia ucha mungu.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe..29.11.2024
No comments:
Post a Comment