Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Mizengo Pinda akihutubia kama mgeni rasmi katika kongamano la wanaume lililofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Usevya Novemba 23, 2024 katika halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amewataka wazazi wote nchini kuwalea watoto kwa usawa bila ubaguzi ili kuepuka na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Naibu Waziri Pinda ametoa wito huo Novemba 23, 2024 alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la wanaume likiongozwa na mada isemayo Wanaume na Ukatili wa Kijinsia lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Usevya.
"Wakati tunawaangalia watoto wa kike kwa umuhimu wao tumesahau kundi lingine la watoto wakiume hatujawawekea umaalumu katika kuwatunza na kuwalea" amesema Mhe. Pinda
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema Ukatili wa Kijinsia unaongezeka kutokana na wanaume kushindwa kutimiza wajibu na majukumu yao katika familia.
Kadhalika Shaban Rashid mkazi wa Usevya ameshukuru kufanyika kwa kongamano hili akiamini litakwenda kubadili mtazamo hasi wa wanaume dhidi ya Wanawake.
No comments:
Post a Comment