Habari za Punde

Waziri Mhe.Tabia Azindua Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliani Zanzibar

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  akizindua Jumuiya ya Maofisa Habari na Mawasiliano  Zanzibar (ZICOO) katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  amewataka Maofisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kutoa taarifa za utendaji wa Serikali kwa wananchi .

Hayo ameyaeleza huko katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini wakati wa uzinduzi  wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano Zanzibar (ZICCO).
Amesema maafisa wa habari wa serikali na watu binafsi wanajukumu la kuhakikisha kuwa wananchi  wanapata habari za Taasisi zao  pamoja na huduma zinazotolewa katika taasisi hizo.

" Kuna miradi mingi ya maendeleo inafanyika katika Taasisi lakini  wananchi hawaelewi kutokana na Taasisi hizo kukaa kimnya bila kuijulisha jamii"amesema Mhe, Tabia .

Aidha amesema  kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu 18 (1 na 2)kinatoa uhuru kila mtu anahaki ya kupokea na kutoa habari na kinaonyesha haki ya raia kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali yanayofanyika nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi.

Amefahamisha kwamba kuwepo kwa Jumuiya hiyo kutasaidia  kutekeleza malengo ya kuundwa kwake ili jamii ipate taarifa ya maendeleo  yanayotekelezwa na Serikali  yao sambamba na kupata fursa ya kuzieleza changamoto zao.

Amesema  kuna baadhi ya Taasisi hazitumii vyombo vya habari au maafisa habari  jambo ambalo linasababisha wananchi kutoele juu ya upatikanaji wa huduma zinazotolewa na Taasisi hizo.

Amefahamisha kuwa  kutowashirikisha ipasavyo Maafisa Habari katika  vikao vya utendaji kunachangia kuwadumaza kwa kutopata taarifa za kuwapa wananchi.

Ameeleza kwamba kuanzisha Jumuiya  ni hatua moja lakini jambo la muhimu kuhakikisha Jumuiya hiyo inadumu na kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Nae  Katibu wa Itikafi Uwenezi wa Chama cha Mapinduzi  Ndugu Khamis Mbeto Khamis amesema Serikali ya awamu ya nane imefanya miradi mingi lakini maafisa habari hawaitangazi jambo ambalo wananchi wanashindwa kujuwa.

Amesema nchi yoyote inajengwa na Maafisa Habari hivyo Watendaji wakuu  iko haja ya kubadilika kwa kutumia nafasi ya kuyatangaza maendeleo ya nchi.

"kuna miradi bado haijatangazwa kwa  wananchi ili kuitambuwe ikiwemo Vwanja vya mpira,Bandari, Barabara, barabara za juu (flyover), na kwengine mwingi lakini hamtangazi kwa jamii wakajuwa "amesema Mbeti.

kwa upande wa Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Habari na Mawasiliano Zanzibar  (ZICOO) Makame Khamis Mohamed amesema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni  kuwaweka pamoja maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania  ili  kuimarisha umoja, uwazi na uwajibikaji kupitia Wizara zao,  sambamba na kuongeza umahiri na uweledi katika kazi zao.

amesema Jumuiya hiyo imesaidia kupata fursa za kuelezea changamoto zinazowakabili maofisa hao ikiwemo kutopata taarifa sahihi na kwa wakati katika Taasisi zao jambo ambalo lilikuwa linakwamisha utekelezaji wa majukumu yao.

hata hivyo amefahamisha kuwa kutokana na hali ya Maofisa Habari katika Taasisi haiyendani na hali ya sasa ambayo inaviza utekelezaji wa majukumu sambamba na kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara yatasaidia kuengeza uweledi wa kazi zao.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  akizungumza na Maofisa Habari na Mawasiliano  Zanzibar (ZICOO) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  akimkabidhi Tunzo  Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Habari Maelezo Hassan Khatib Hassan (katikati)  Afisa Habari Raya Hamad wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Maofisa Habari na Mawasiliano  Zanzibar (ZICOO) huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.
Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Maofisa Habari na  Mawasiliano  Zanzibar (ZICOO) wakimzikiliza Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita  (hayupo pichani  ) katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.