Habari za Punde

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR- PEMBA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amewasili Kisiwani Pemba kwa Shughuli za Kikazi. 


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi zanzibar Kisiwani Pemba kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kusimamia majukumu yao ili kumsaidia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Mwinyi kutekeleza ahadi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar

Ameyasema hayo katika Kikao kazi  kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya makamu wa pili wa rais tibirinzi kilicho washirikisha wakuu wa mikoa na wilaya, maafisa wadhamin pamoja na wakurugenzi wa mabaraza ya miji, manispaa na Halmashauri.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha inawaletea wananchi wake maendeleo kwa kuwafikishia huduma bora na stahiki katika maeneo yanayo wazunguka pamoja na kuzitatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi hao

Makamunwa Pili wa Rais amewasisitiza  viongozi hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana na kupeana maelekezo chanya yenye mustakbali wa kufikia maendeleo endelevu nchini.

Nae wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe.Massoud Ali Moh'd amewataka viongozi hao kuelekeza nguvu zao katika kuitumikia Serikali ili iwezekutimiza maelengo yake iliyojiwekea ikiwemo suala zima la maendeleo.

Wakati huo huo Makamu ya wa Pili wa Rais amefanya ziara ya kukagua uwanja wa mpira wa Gombani ambao unaofanyiwa ukarabati mkubwa ili kuweza kuwa na hadhi na vigezo vya Kimataifa na unatarajiwa kufanyika sherehe za miaka 61 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Mhe.Hemed amewataka wakandarasi wanaojenga uwanja huo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanamaliza kwa wakati uliopangwa na ubora wa hali ya juu ili kuweza kudumu kwa muda mrefu.

Nae mshauri elekezi kutoka wakala wa Majengo ZBA Ndugu SAID MALIK amesema wamepokea maelekezo yote waliyopewa na Mhe. Makamu wa Pili ikiwemo la kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza ndani ya wakati uliopangwa.

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe ..09 / 12 / 2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.